Kipindi hichi kumebaki sehemu ya ujana na nafsi bado ni yenye kuvutikiwa na matamanio. Hapa kuna mapambano mazuri pia, hata kama umri unapunguza hamu kwa mambo ya kipuuzi.

Mtu wa wastani anatakiwa kutosheka na mwanga wa mvi zinazomwangazia njia ya safari yake. Anatakiwa kutumia mvuto wa matamanio uliyobaki kwa njia ya kufaidi, lakini sio sawa kama anavyofaidi kijana. ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) amesema kuhusu mtu ambaye amemwingilia mke wake wakati wa hedhi:

“Ikiwa ni mwanzoni mwa hedhi basi anatakiwa kutoa dinari moja na ikiwa ni mwishoni mwa hedhi basi atoe nusu ya dinari.”

Hili ni kwa sababu ametoka punde tu kufanya naye jimaa kabla ya kuingia hedhini na kwa sababu hiyo hapewi udhuru tofauti na mtu aliyesubiri jimaa kwa muda mrefu na hivyo akawa amefanya naye jimaa mwishoni mwa hedhi yake. Kwa ajili hiyo ndio maana akatoa kafara kidogo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin al-Jawziy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyh-un-Naa’im al-Ghamr ´alaa Mawswim-il-´Umr, uk. 65-66
  • Imechapishwa: 15/02/2017