727- Abul-Ja´d adh-Dhwamriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuacha ijumaa tatu kwa ajili ya hali ya kutozijali[1], basi Allaah atapiga muhuri katika moyo wake.”[2]

Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, at-Tirmidhiy ambaye amesema ni nzuri, Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh”, Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” na al-Haakim aliyesema:

“Ni Swahiyh juu ya sharti za Muslim.”

Katika upokezi wa Ibn Khuzaymah na al-Haakim imekuja:

“Yule mwenye kuacha ijumaa tatu pasi na udhuru ni mnafiki.”[3]

Abul-Ja´d jina lake ni Adra´. Kuna maoni mengine yanayosema anaitwa Junaadah. al-Karaabiysiy amesema kuwa jina lake ni ´Umar bin Abiy Bakr. at-Tirmidhiy amesema:

“Nilimuuliza Muhammad (al-Bukhaariy) kuhusu jina la Abul-Ja´d lakini alikuwa hajui.”

[1] Kutokana na uchache wa kuzitilia umuhimu, sio kwa sababu anazidharau. Kwa sababu kuzidharau faradhi za Allaah (Ta´ala) ni ukafiri na kuritadi. Ni kufuru ya kimoyo.

[2] Nzuri.

[3] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/450-451)
  • Imechapishwa: 26/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswiyr-ud-Diyn al-Albaaniy