115- Abu Mas´uud al-Badriy amesema:

“Bwana mmoja alimjia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akimuomba mnyama wa kupanda ambapo akasema: “Nimemchosha.” Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Mwendee fulani.” Bwana yule akamwendea na akapata kipando. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Yeyote atakayeelekeza kheri basi ana mfano wa ujira wa yule mwenye kuifanya.”[1]

Ameipokea Muslim, Abu Daawuud na at-Tirmidhiy[2].

[1] Swahiyh.

[2] Tamko ni lake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/157)
  • Imechapishwa: 03/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy