Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

677- Sahl bin Sa´d (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu hawatoacha kuwa juu ya kheri muda wa kuwa wanaharakisha kukata swawm.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

678- at-Tirmidhiy amempokea Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) amesema: “Waja wangu ninaowapenda zaidi ni wale wanaoharakisha kukata swawm.”[2]

MAELEZO

Hadiyth ya Sahl bin Sa´d (Radhiya Allaahu ´anh) inajulisha kwamba kila ambavo mtu ataharakisha kukata swawm baada ya kuhakikisha kuzama kwa jua au akawa na dhana yenye nguvu kwamba limekwishazama kwa sababu ya mawingu na mfano wake, basi ndio bora zaidi. Kwa sababu ya kuharakisha kutendea kazi ruhusa ya Allaah (´Azza wa Jall). Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu hawatoacha kuwa juu ya kheri muda wa kuwa wanaharakisha kukata swawm.”

Lakini ukiwa uko nyumbani na hulioni jua na mwadhini ni mwaminifu, basi fanyia kazi adhaana yake. Lakini ukiwa nchikavu na unaliona jua vizuri, basi usikate swawm mpaka lizame hata kama mwadhini ataadhini.

[1] al-Bukhaariy (1957) na Muslim (1098).

[2] at-Tirmidhiy (700). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (700).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mukhtaswar ´alaa Buluugh-il-Maraam (2/408-410)
  • Imechapishwa: 24/04/2020