04. Hadiyth ”Mwenye kuchukua njia akifuta elimu katika njia hiyo… “

70- Abud-Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh) amesema: ”Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Mwenye kuchukua njia akifuta elimu katika njia hiyo, basi Allaah atamsahilishia njia ya kuelekea Peponi. Hakika Malaika huziweka mbawa zao juu ya mwanafunzi wakiridhia kile anachokifanya. Hakika mwanachuoni anaombewa msamaha na vyote vilivyomo mbinguni na ardhini mpaka nyangumi ndani ya maji. Ubora wa mwanachuoni ukilinganisha na yule mwenye kufanya ´ibaadah ni kama ubora wa mwezi ukilinganisha na nyota zengine. Wanachuoni ndio warithi wa Mitume. Hakika Mitume hawakurithi dinari wala dirhamu, lakini wamerithi elimu. Mwenye kuichuma basi amejichumia fungu nono.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” na al-Bayhaqiy.

[1] Nzuri pitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/136-137)
  • Imechapishwa: 13/09/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy