04. Hadiyth “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali nne baada ya jua kupinduka… “

587- ´Abdullaah bin as-Saa-ib (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali nne baada ya jua kupinduka na kabla ya Dhuhr na akasema: “Hicho ni kipindi ambacho hufunguliwa milango ya mbingu. Hivyo napenda kipindi hicho yanyanyuliwe matendo yangu.”[1]

Ameipokea Ahmad na at-Tirmidhiy ambaye amesema:

“Hadiyth ni nzuri na geni.”[2]

[1] Swahiyh.

[2] Kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja inafahamisha kwamba alikuwa haziswali kabla ya swalah ya ijumaa. Ni ufahamu ambao unatakiwa kuzingatiwa kwa kuthibiti kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapofika tu msikitini basi huketi moja kwa moja juu ya mimbari pasi na kipambanuzi. Kisha anapoketi chini Bilaal hutoa adhaana. Baada ya kumalizika adhaana ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) huanza kutoa Khutbah. Kwa msemo mwingine ni kwamba hakukuweko wakati wa kuswali Rak´ah mbili, sembuse nne, katika Sunnah za kinabii. Je, hujafika wakati wa wale wanaofuata kichwa mchunga kutambua uhakika huu na kwamba swalah ambayo haikufungamana inaswaliwa kabla ya adhaana na kabla ya jua kupinduka? Tazama upambanuzi huu katika kijitabu changu ”al-Ajwibah an-Naafi´ah”.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/381)
  • Imechapishwa: 14/01/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy