719- Amepokea vilevile kupitia kwa Jaabir ambaye amesema:

“´Abdullaah bin Mas´uud aliingia msikitini na huku Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anakhutubu. Akakaa karibu na Ubayy bin Ka´b ambapo akamuuliza kitu au akasema kitu. Ubayy hakujibu kitu jambo ambalo lilimfanya Ibn Mas´uud kudhani kwamba alikuwa amekasirika. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomaliza swalah yake Ibn Mas´uud akasema: “Ee Ubayy! Ni kwa nini hukunijibu?” Akasema: “Wewe hukuhudhuria swalah ya ijumaa pamoja nasi.” Akasema: “Ulizungumza na huku Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anatoa Khutbah.” Ibn Mas´uud akasimama, akaingia kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumueleza yaliyotokea. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ubayy amesema kweli. Ubayy amesema kweli. Mtii Ubayy!”[1]

Ameipokea Abu Ya´laa´ kwa mlolongo wa wapokezi mzuri na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh”.

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/448)
  • Imechapishwa: 14/01/2018