1082- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kufunga sio kuacha kula na kunywa. Funga kikweli ni mtu kuacha maneno na ya kipuuzi na yasiyokuwa na maana. Mtu akikutukana au akakufanyia ujinga, basi amwambie: “Mimi nimefunga. Mimi nimefunga.”[1]

Ameipokea Ibn Khuzaymah, Ibn Hibbaan na al-Haakim aliyesema:

“Ni Swahiyh juu ya sharti za Muslim.”

Katika upokezi wa Ibn Khuzaymah imekuja kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Usitukane ilihali umefunga. Mtu akikutukana basi mwambie: “Mimi nimefunga.” Na kama ulikuwa umesimama basi keti chini.”[2]

[1] Swahiyh.

[2] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/625)
  • Imechapishwa: 24/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy