04. Hadiyth “Inapokuwa siku ya ijumaa Malaika hukaa kwenye milango ya misikiti na wanawaandika wale watu… “

711- Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Inapokuwa siku ya ijumaa Malaika hukaa kwenye milango ya misikiti na wanawaandika wale watu wanaokuja kwa mujibu wa ngazi zao. Mmoja anazingatia kutoa ngamia. Mwingine anazingatiwa kutoa ng´ombe. Mwingine anazingatiwa kutoa kondoo. Mwingine anazingatiwa kutoa kuku. Mwingine anazingatiwa kutoa yai. Pindi muamini anapoadhini na imamu akaketi chini kwenye mimbari, hufunga madaftari na wakaingia msikitini kwa ajili ya kusikiliza ukumbusho.”[1]

Ameipokea Ahmad kwa mlolongo wa wapokezi mzuri.

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/445)
  • Imechapishwa: 25/01/2018