04. Hadiyth “Hawakupotea watu… “

141- Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hawakupotea watu baada ya uongofu walikuwemo isipokuwa kulianza ubishi kwanza:

Kisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasoma Aayah isemayo:

مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ

”Hawakukupigia mfano huo isipokuwa tu kutaka kubisha. Bali wao ni watu mahasimu.”[1][2]

Ameipokea at-Tirmidhiy, Ibn Maajah na Ibn Abiyd-Dunyaa katika ”Kitaab-us-Swamt” na wengineo. at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”[3]

[1] 43:58

[2] Nzuri.

[3] al-Haakim pia ameisahihisha na ad-Dhahabiy akaafikiana naye. Hata hivyo ni nzuri tu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/169-170)
  • Imechapishwa: 07/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy