04. Hadiyth “Hakika shaytwaan amekata tamaa… “

40- Ibn ´Abbaas amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwatolea watu Khutbah katika hijjah ya kuaga akasema: “Hakika shaytwaan amekata tamaa ya yeye kuabudiwa katika ardhi yenu. Lakini ameridhia kutiiwa katika yasiyokuwa hayo katika mambo ambayo mnayadharau katika matendo yenu. Tahadharini! Hakika mimi nimeacha kati yenu yale ambayo endapo mtashikamana nacho basi kamwe hamtopotea; Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake.”[1]

Ameipokea al-Haakim ambaye amesema:

“Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh. al-Bukhaariy ameijengea hoja kwa ´Ikrimah na Muslim ameijengea hoja kwa Abu Uways. Inayo msingi katika “as-Swahiyh”.”

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/124-125)
  • Imechapishwa: 26/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy