04. Hadiyth “Hakika kile ninachochelea juu yenu ni upotofu wa matamanio… “

52- Abu Barzah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika kile ninachochelea juu yenu ni upotofu wa matamanio ndani ya tumbo na tupu zenu na matamanio yenye kupotosha.”[1]

 Ameipokea Ahmad, al-Bazzaar na at-Twabaraaniy. Baadhi ya cheni zake wapokezi wake ni waaminifu.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/130)
  • Imechapishwa: 27/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy