04. Hadiyth “Haitovuka miguu ya mja siku ya Qiyaamah mpaka… “

126- Abu Barzah al-Aslamiy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Haitovuka miguu ya mja siku ya Qiyaamah mpaka aulizwe juu ya mambo mane: umri wake aliuteketeza katika mambo gani, elimu yake aliifanyia nini, mali yake aliipata kivipi na akaitumia wapi na mwili wake aliutumia vipi?”[1]

Ameipokea at-Tirmidhiy aliyesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/162)
  • Imechapishwa: 05/05/2020