04. Hadiyth ”Awe mbali yule ambaye itamfikia Ramadhaan… “


995- Ka´b bin `Ujrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hudhurieni kwenye mimbari!” ambapo tukahudhuria. Alipopanda daraja ya kwanza akasema ”Aamiyn.” Alipopanda daraja ya pili akasema ”Aamiyn.” Alipopanda daraja ya tatu akasema ”Aamiyn.” Alipotua tukasema: ”Ee Mtume wa Allaah!  Leo tumekusikia ukisema kitu ambacho hatujapatapo kukusikia ukikisema.” Akasema: ”Jibriyl ameniteremshia na kusema: ”Awe mbali yule ambaye itamfikia Ramadhaan na asisamehewe.” Nikasema: ”Aamiyn.” Nilipopanda daraja ya pili akasema: ”Awe mbali yule ambaye jina lako litatajwa mbele yake na asikuswalie.” Nikasema: ”Aamiyn.” Nilipopanda daraja ya tatu akasema: ”Awe mbali yule ambaye atadiriki uzee wa wazazi wake wawili, au uzee wa mmoja katika wao, na asiingie Peponi kwa ajili yao.”[1]

al-Haakim amesema:

”Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.”

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/583)
  • Imechapishwa: 12/05/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy