04. Hadiyth “Allaah ampambe mtu ambaye amesikia maneno yangu… “

92- Jubayr bin Mut´im amesema:

“Nilimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Khayf huko Minaa akisema: “Allaah ampambe mtu ambaye amesikia maneno yangu ambapo akayahifadhi, akayaelewa kisha akamfikishia yule ambaye bado hajayasikia. Huenda ambaye amebeba uelewa yeye mwenyewe hana uelewa. Huenda ambaye amebeba uelewa akamfikishia ambaye ana uelewa zaidi kuliko yeye. Moyo wa muumini hauyaonei wivu kwa mambo: kumtakasia kitendo cha Allaah, kumnasihi watawala wa waislamu kulazimiana na mkusanyiko. Kwa sababu kuwaombea du´aa wao kunawazunguka walio nyuma yake wote.”[1]

Ameipokea Ahmad, Ibn Maajah na at-Twabaraaniy katika “al-Kabiyr” kwa ufupi na kwa urefu.

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/148)
  • Imechapishwa: 01/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy