Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amepanga thawabu tukufu kwa ambaye atasimamia kazi hii. Sahl bin Sa´d (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh):

“Naapa kwa Allaah! Kule Allaah kumwongoza mtu mmoja kupitia kwako ni bora kwako kuliko ngamia wekundu.”[1]

Ngamia wekundu walikuwa mali ya yenye thamani zaidi kwa waarabu na ilikuwa inapigiwa mfano kuonyesha thamani ya kitu na kwamba hakuna kitukufu zaidi kushinda kitu hicho[2]. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote anayelingania katika uongofu basi anapata ujira mfano wa yule mwenye kumfuata pasi na kupungua chochote katika ujira wao. Na yeyote anayelingania katika upotevu basi anapata dhambi mfano wa yule mwenye kumfuata pasi na kupungua chochote katika dhambi zao.”[3]

Abu Mas´uud al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote anayejulisha katika jambo basi ana ujira wa mfano wa mtendaji.”[4]

Hebu waislamu washindane katika fadhilah hii na watwae thawabu hii. Hebu washindane wale wenye kushindana!

[1] al-Bukhaariy (309) na Muslim (405).

[2] Tazama ”Sharh Swahiyh Muslim” (15/178) ya an-Nawawiy.

[3] Muslim (2674).

[4] Muslim (1893).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 8-9
  • Imechapishwa: 29/07/2022