04. Dalili ya pili kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

2- Shaykh Abul-Fath Muhammad bin ´Abdil-Baaqiy bin Ahmad bin Sulaymaan ametuhadithia: Hamd bin Ahmad al-Haddaad ametuhadithia: Haafidhw Abu Nu´aym Ahmad bin ´Abdillaah ametueleza: ´Abdullaah bin Ja´far bin Ahmad bin Faaris ametueleza: Yuunus bin Habiyb ametuhadithia: Abu Daawuuud at-Twayaalisiy ametuhadithia: Harb bin Shaddaad na Abaan bin Yaziyd ametuhadithia, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa Hilaal bin Abiy Maymuunah, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Yasaar, kutoka kwa Mu´aawiyah bin al-Hakam as-Sulamiy aliyesema:

“Nilikuwa na kondoo kati ya Uhud na al-Jawaaniyyah wanaochungwa na kijakazi wangu. Siku moja akaja mbwa mwitu na akamchukua kondoo kutoka kwake. Mimi ni mwanaadamu wa kawaida ambaye hukasirika kama wanavyokasirika watu wengine. Nikaunyanyua mkono wangu na kumpiga kofi. Nikamwendea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumweleza yaliyopitika. Nikasikitika na kumwambia: “Ee Mtume wa Allaah! Si nimwache huru?” Akasema: “Mwite.”Nikamwita. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: “Allaah yuko wapi?” Akajibu: “Juu ya mbingu.” Akamuuliza: “Mimi ni nani?” Akajibu: “Wewe ni Mtume wa Allaah.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Mwache huru. Kwani hakika ni muumini.”[1]

Hadiyth ni Swahiyh. Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake, Maalik katika “al-Muwattwa” na maimamu wengineo (Rahimahu Allaah).

[1] Muslim (537), Abu Daawuud (930), an-Nasaa’iy (3/13), Maalik (2/776), Ibn Abiy ´Aaswim (479), al-Bayhaqiy, uk. 422, Ahmad (5/447), Abu Daawuud at-Twayaalisiy (1105) na Ibn Khuzaymah katika ”at-Tawhiyd”, uk. 121.

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 69
  • Imechapishwa: 26/02/2018