04. Dalili juu ya mguu wa Allaah 4

04- ´Aliy bin ´Abdillaah bin Muyassir ametuhadthia: Abul-Ash´ath Ahmad bin al-Miqdaam ametuhadthia: Muhammad bin ´Abdir-Rahmaan at-Twafaawiy: Ayyuub ametuhadthia, kutoka kwa Muhammad, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Pepo na Moto vilizozana ambapo Moto ukasema: “Ndani yangu wanaingia wakandamizaji na wenye kiburi.” Pepo nayo ikasema: “Ndani yangu wanaingia watu wadhaifu na wale masikini.” Ndipo Allaah (´Azza wa Jall) akasema: “Wewe ni adhabu Yangu ambayo namsibu yule Ninayemtaka.” Akasema kuiambia Pepo: “Wewe ni huruma Yangu ambayo namsibu yule Ninayemtaka. Kila mmoja wenu atajazwa.” Itapofika siku ya Qiyaamah basi Allaah (´Azza wa Jall) hatomdhulumu yeyote katika waja Wake kitu chochote. Kutatupwa Motoni na useme:

هَلْ مِن مَّزِيدٍ

“Hakuna zaidi?”[1]

Mpaka Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) aweke unyayo Wake. Hapo ndipo utajaa, ukusanyike na useme: “Tosha, tosha.”

[1] 50:30

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 39-40
  • Imechapishwa: 18/10/2017