Swali 4: Baadhi ya watu wanakula na huku kunaadhiniwa adhaana ya pili ya Fajr katika mwezi wa Ramadhaan. Ni upi usahihi wa funga zao?
Jibu: Ikiwa muadhini anaadhini pale tu kunapochomoza kwa alfajiri basi ni lazima kwake kujizuia kuanzia pale anapomsikia muadhini. Kwa hiyo asile na wala asinywe. Lakini akiwa anaadhini kwa kudhani – na si kwa uhakika – kuwa Fajr imekwishaingia (kama hali ilivyo hii leo), basi anaruhusiwa kula na kunywa mpaka pale muadhini atakapomaliza kuadhini.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 12
- Imechapishwa: 10/04/2021