04. Allaah ndiye hukisimamia kipomoko kwenye kifuko cha uzazi


… akamtia sura tumboni mwa mama yake… – Allaah (Ta´ala) amesema:

هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاءُ

“Yeye ndiye aliyekutieni sura katika matumbo ya uzazi vile Atakavyo.”[1]

خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ الْأَنْعَامِ ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ ۚ يَخْلُقُكُمْ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ خَلْقًا مِّن بَعْدِ خَلْقٍ فِي ظُلُمَاتٍ ثَلَاثٍ

“Amekuumbeni kutokamana na nafsi moja, kisha akamfanya humo mkewe na akakuteremshieni katika wanyama wa mifugo jozi nane; anakuumbeni katika matumbo ya mama zenu umbo baada ya umbo, katika viza vitatu.”[2]

Visa vitatu kunakusudiwa giza la tumboni, giza kwenye kifuko cha uzazi na giza la kondo la nyuma linalomfunika mtoto. Ni nani anayepanga mpangilio mzuri huu katika viza hivi? Si mwingine isipokuwa ni Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye anayefanya hayo kupitia Malaika anayemtumiliza kwa kipomoko tumboni mwa mama yake. Anamwamrisha aandike mambo manne: riziki, muda wa kuishi, matendo na kama mtoto huyo atakuwa mla khasara au mwenye furaha. Ni nani ambaye humtoa nje mtoto huyu katika viza hivi na kumleta katika maisha haya? Ni nani ambaye humwendeleza? Ni nani ambaye humpa chakula anapokuwa katika viza hivi? Si mwingine isipokuwa ni Allaah (Subhaanahu wa Ta´al).

[1] 3:6

[2] 39:6

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 13
  • Imechapishwa: 30/06/2021