05. al-Ikhwaan al-Muslimuun wanarekebisha tabia na wanapuuza ´Aqiydah

Tatu ni kwamba al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) alinukuu maneno ya Sayyid Qutwub kwa lengo la kutumia hoja dhidi ya wale madaktari ambao walidai kwamba watu hawana haja ya masomo ya ´Aqiydah na kwamba badala yake wanahitajia kujifunza tabia. Daktari huyo amesema:

“Waislamu wa leo hawana tena haja ya kuweka muda wao zaidi juu ya kusoma masomo ya ´Aqiydah. Pamoja na tamaduni mbalimbali za waislamu wamekuwa ni wenye kufahamu kiasi kikubwa cha ´Aqiydah hii. Kitu wanachohitajia sana ni utendaji. Hata hivyo ni jambo lisilowezekana kutekelezwa kwa ´Aqiydah na akili peke yake. Wanachohitajia ni tabia.”[1]

Hii ni njia ya chama, nacho si kingine ni chama cha al-Ikhwaan al-Muslimuun. Wanatilia umuhimu kurekebisha tabia ilioharibika na wanapuuza ´Aqiydah. Bali wanamgombeza yule mwenye kuibainisha ´Aqiydah au akataka kuwakaripia wao au ´Aqiydah za wengineo.

[1] Baatwin-ul-Ithm, uk. 64

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 21/10/2018