04. Adabu ya nne: kula kidogo cha halali na unyenyekevu

Ibn Jamaa´ah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Miongoni mwa sababu kubwa zinazomsaidia mtu na kujishughulisha, kufahamu na kutosemwa vibaya ni kula kiasi kidogo tu cha halali.

ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Sijawahi kushiba tangu miaka kumi na sita.”

Hilo ni kwa sababu kula sana kunapelekea kunywa sana na kunywa sana kunapelekea kulala, uchovu na uvivu. Jambo hili lina machukizo ya Kishari´ah na kujiweka katika ukhatari wa kimwili. Kama ilivyosema:

“Hakika maradhi mengi yanayopatikana yanatokamana na chakula na vinywaji. Hakukuona yeyote katika mawalii na maimamu wa ulimwengu wakisifika na kutapwa kwa kula sana…

Lau kusingelikuwepo madhara ya kula na kunywa sana zaidi ya ile haja inayopatikana ya kuingia choni sana, basi ilikuwa inatakikana kwa mwerevu ajichunge kutokamana na hilo.”[1]

Ni juu ya mwanafunzi awe na unyenyekevu katika mambo yake yote na ale kile cha halali katika vyakula, vinjwaji vyake, mavazi, makazi yake na katika mambo mengiene yote anayoyahitaji yeye na familia yake. Anatakiwa ausafishe moyo wake na autengeneze na kuipokea elimu, kuupa mwanga na kuunufaisha…

Mwanafunzi anatakiwa kuwaiga wale wanachuoni wema waliotangulia ambapo walikuwa wakinyenyekea katika mengi ambayo walikuwa wakifutu ya kwamba yanajuzu. Kiigizo bora wa kuigwa katika hayo ni Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo hakula tende aliokutana nayo barabarani kwa kuchelea isije kuwa ni swadaqah. Hakika wanachuoni wanatakiwa waigwe na ichukuliwe elimu kutoka kwao. Endapo wao hawatotumia unyenyekevu, utatumiwa na nani?

[1] Tadkhirat-us-Saamiy´ wal-Mutakallim”, uk. 74

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Sa´iyd Raslaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadab Twaalib-ul-´Ilm, uk. 43-70
  • Imechapishwa: 23/04/2017