03. Yanayopelekea kwa kufanya mambo kumi haya

Mambo yakishakuwa namna hii ya kwamba hukumu yake duniani ni kuwa hasamehewi na Aakhirah ni mwenye kudumishwa Motoni milele na Pepo ni haramu kwake, kuna hukumu kadhaa zinazopelekea hapa duniani. Baadhi ya hukumu hizo ni hizi zifuatazo:

1- Mke wake anatengana naye – ikiwa ameshaoa. Inatakiwa kumtenganisha baina yake yeye na mke wake. Isipokuwa ikiwa kama atatubu. Wanatenganishwa kwa sababu yeye mke wake ni muislamu na mume ni kafiri. Haifai kwa mwanamke wa Kiislamu akabaki chini ya usimamizi wa kafiri. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

“Wao si [wake] halali kwao na wala wao si [waume] halali kwao.”[1]

Bi maana makafiri.

وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ

“Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini.”[2]

2 – Haitakiwi kumswalia wala kumuosha wakati atapokufa.

3 – Hazikwi kwenye makaburi ya waislamu.

4 – Asiingie Makkah. Haijuzu kwa mshirikina kuingia Makkah. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَـٰذَا

“Enyi mlioamini! Hakika washirikiana ni najisi, basi wasikaribie al-Masjid al-Haraam baada ya mwaka wao huu.”[3]

5 – Hana haki ya kurithi wala ya kurithiwa. Ikiwa mke na watoto wake ni waislamu wasimrithi. Mali yake inaenda kwenye sanduku la waislamu. Isipokuwa ikiwa kama ana mtoto ambaye ni kafiri, ana haki ya kumrithi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muislamu hamrithi kafiri wala kafiri hamrithi muislamu.”[4]

Kwa hivyo tunapata kuona kuwa akifanya moja katika vichenguzi hivi  na akaendelea juu yake, basi inapelekea katika hukumu kadhaa; haoshwi, haswaliwi, hazikwi makaburini pamoja na waislamu, harithi na wala harithiwi, mke wake anatenganishwa naye na haingii Makkah. Jengine ni kuwa akifa juu ya hilo dhambi yake haisamehewi na Pepo ni haramu kwake. Aidha ni katika watu wa Motoni ambaye atadumishwa humo milele.

[1] 63:10

[2] 02:221

[3] 09:28

[4] al-Bukhaariy (6764) na Muslim (1614).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tabswiyr-ul-Anaam bisharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 13-14
  • Imechapishwa: 09/04/2023