Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ

“Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa kufunga kama ilivyofaradhishwa kwa waliokuwa kabla yenu.”[1]

Hapa Allaah (´Azza wa Jall) anatukhabarisha kwamba ametufaradhishia na kutuwajibishia swawm kama alivyoiwajibisha kwa wale ambao walikuwa kabla yetu. Allaah aliwawajibishia wale ambao walikuwa kabla yetu kufunga siku tatu kila mwezi na siku ya ´Aashuuraa´. Imesemekana vilevile kuwa Allaah aliwawajibishia wana wa israaiyl kufunga Ramadhaan. Halafu wakaongeza siku kumi na hapo ndipo swawm ikawa siku arubaini. Kisha mmoja katika wafalme wao akawa mgonjwa ambapo akawa ameweka nadhiri kuongeza siku kumi endapo atapona. Kitu ambacho alikifanya. Wakawa wanafunga siku khamsini. Ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba nyongeza zao hizi ilikuwa ni kosa.

Hapo ndipo Allaah (´Azza wa Jall) akauwajibishia Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufunga mwezi huu mtukufu. Kwa sababu Allaah ameteremsha Qur-aan ndani yake. Kwa hivyo mwezi huu unatakiwa kufungwa kwa ajili ya kuishukuru neema ya Qur-aan.

[1] 02:183

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 7-9
  • Imechapishwa: 02/06/2017