Iwapo umeelewa maana, basi hapa tutazungumzia uchambuzi wake kisarufi kijumla. Wanazuoni (Rahimahumu Allaah) wametilia umuhimu uchambuzi wa kisarufi wa maana ya ´hapana mungu isipokuwa Allaah`. Kwa hivyo wamesema kuwa ´hapana` ni makanusho yaliyotangulizwa yanayofuatiwa na ´haki` ambapo maana yake inakuwa ´hapana mungu wa haki`.

Mungu ni yule mwabudiwa, mwenye kuadhimishwa na kukusudiwa na mioyo, hali ya kuwa na matumaini kwake katika kufikia manufaa au kuyazuia madhara. Ni makosa kusema kuwa maana yake ni ´hapana kilichopo au mwabudiwa` peke yake. Kwa kuwa kuna masanamu, makaburi na vinginevyo vyenye kuabudiwa. Lakini hata hivyo mwenye kuabudiwa kwa haki ni Allaah pekee. Vingine vyote badala Yake ni vyenye kuabudiwa kwa batili na kuabudiwa kwao ni batili. Haya ndio yanapelekewa na shahaadah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´naa laa ilaaha illa Allaah, uk. 16
  • Imechapishwa: 23/09/2023