05 – Tofauti kati ya matendo mema na matendo mabaya

03 – Tofauti kati ya matendo mema na mabaya

Qur-aan tukufu imebainisha kuwa matendo mema ni yale yaliyotimiza sharti tatu. Ikikosekana sharti moja, basi hayatomfaa kitu mwenye nayo siku ya Qiyaamah:

1 – Kitendo hicho kiwe kinaafikiana na yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[1]. Allaah amesema:

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا

“Yale anayokupeni Mtume, basi yachukueni, na yale anayokukatazani, yaacheni.”[2]

مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ

“Atakayemtii Mtume, basi kwa hakika amemtii Allaah.”[3]

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي

“Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi.””[4]

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ

“Je, wanao washirika waliowaamuru dini yale ambayo Allaah hakuyaidhinisha?”[5]

أَمْ عَلَى اللَّـهِ تَفْتَرُونَ

“.. au mnamtungia Allaah uongo?”[6]

2 – Yafanywe kwa ajili ya Allaah (Ta´ala) pekee. Amesema:

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ

“Hawakuamrishwa jengine isipokuwa wamwabudu Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini.”[7]

قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ وَأُمِرْتُ لِأَنْ أَكُونَ أَوَّلَ الْمُسْلِمِينَ قُلْ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ قُلِ اللَّـهَ أَعْبُدُ مُخْلِصًا لَّهُ دِينِي فَاعْبُدُوا مَا شِئْتُم مِّن دُونِهِ ۗ قُلْ إِنَّ الْخَاسِرِينَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ أَلَا ذَٰلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ

“Sema: “Hakika mimi nimeamrishwa nimwabudu Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini na nimeamrishwa kuwa niwe wa kwanza wa waislamu.” Sema: “Hakika mimi nachelea nikimwasi Mola wangu nitapata adhabu ya siku kubwa.” Sema: “Allaah pekee ndiye ninayemwabudu hali ya kumtakasia Yeye dini, hivyo basi abuduni mnayotaka badala Yake.” Sema: “Hakika waliokhasirika ni wale waliokhasiri nafsi zao na familia zao siku ya Qiyaamah.” Tanabahi! Huko ndiko kukhasirika kwa wazi kabisa.””[8]

3 – Yawe yamejengwa juu ya msingi wa ´Aqiydah sahihi. Kitendo ni kama dari na ´Aqiydah ni kama msingi. Amesema (Ta´ala):

وَمَنْ يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتِ مِنْ ذَكَرٍ أَوْ أُنْثَى

“Atakayefanya mema akiwa mwanamume au mwanamke… “

Ameyawekea hayo sharti kwa kusema:

وَهُوَ مُؤْمِنٌ

“… hali ya kuwa ni muumini.”[9]

Upande mwingine amesema kuhusu kafiri:

وَقَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا

“Tutayaendea yale waliyoyatenda katika matendo yao, Tuyafanye kama mavumbi yaliyotawanyika.”[10]

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ إِلَّا النَّارُ ۖ وَحَبِطَ مَا صَنَعُوا فِيهَا وَبَاطِلٌ مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ

“Hao ndio wale ambao hawatokuwa na chochote Aakhirah isipokuwa Moto na yataporomoka yale waliyoyafanya duniani nani yenye kubatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.”[11]

Kuna Aayah nyingi mfano wa hizo.

[1] al-Bukhaariy (3/167) na Muslim (3/1343).

[2] 59:07

[3] 04:80

[4] 03:31

[5] 42:21

[6] 10:59

[7] 98:05

[8] 39:11-15

[9] 04:124

[10] 25:23

[11] 11:16

  • Mhusika: Imaam Muhammad Amiyn ash-Shanqiytwiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Islaam diyn al-Kaamil, uk. 13
  • Imechapishwa: 13/06/2023