Maana ya Hadiyth ni kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anamlipa mja kwa matendo yake yote, isipokuwa tu swawm, anawaamrisha Malaika tendo jema moja chini chini wafanye mara kumi. Allaah anaweza kuyalipa matendo zaidi ya hivo kuanzia mara kumi mpaka mara mia saba. Kuhusu swawm Allaah anatoa malipo pasi na hesabu. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ

“Hakika wanaosubiri watalipwa kikamilifu ujira wao bila ya hesabu.”[1]

Hili kwa sababu swawm ni siri baina ya mja na Mola Wake. Katika swawm hakuna kujionyesha. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anajua iwapo mja anafunga kwa ajili Yake kwa imani na kwa kutarajia malipo Yake na kwa kuogopa adhabu Zake.

Nini maana ya swawm ni siri baina ya mja na Mola Wake? Ina maana ya kwamba iwapo utakuwa peke yako na uko na maji, ukasukutua na ukanywa kidogo, Allaah peke yake ndiye atajua hilo. Ukijihifadhi na hilo na ukahakikisha hakuingii kitu ndani, swawm inakuwa ni siri baina yako wewe na Mola Wako. Hakuna mwengine anayejua hilo isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa ajili hiyo ndio maana Allaah anatoa malipo makubwa kwa ajili ya swawm.

[1] 39:10

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Istiqbaal Shahri Ramadhwaan, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 09/06/2017