Haijuzu kwa mtu kuitangulizia Ramadhaan kwa kufunga siku moja au mbili kwa sababu ya kufanya lililo salama zaidi. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiitangulizie Ramadhaan kwa kufunga siku moja au mbili, isipokuwa mtu ambaye alikuwa akifunga swawm. Basi aiendeleze.”

Lakini kama mtu alikuwa na mazowea ya kufunga au alikuwa na deni la siku moja la Ramadhaan iliyopita, basi mtu anayo ruhusa. Kwa mfano mtu ana mazowea ya kufunga jumatatu na siku moja kabla ya Ramadhaan ikaangukia jumatatu, anayo ruhusa ya kufunga. Kwa kuwa hakufunga kwa sababu ya kufanya lililo salama zaidi kwa kuingia kwa mwezi. Hata hivyo amefunga kwa sababu ni katika mazowea yake. Kadhalika kama ana mazowea ya kufunga siku moja na kufungua siku ya kufuata na siku moja au mbili kabla ya Ramadhaan zikaangukia siku ya funga yake – huyu pia hakuna neno kwake kufunga.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mukhtaswar ´alaa Buluugh-il-Maraam (2/406-407)
  • Imechapishwa: 21/04/2020