Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Sharti ya tatu ni kupambanua (Tamyiyz) na kinyume chake ni utoto. Mpaka wake ni miaka saba. Hapo ndipo ataamrishwa kuswali, kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Waamrisheni watoto wenu kuswali wanapofikisha miaka saba, wapigeni wanapofikisha miaka kumi na watenganishe baina yao katika malazi.”[1]

MAELEZO

Kinyume chake ni utoto. Mpaka wake ni miaka saba. Baada ya hapo mtoto anatakiwa kuamrishwa swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Waamrisheni watoto wenu kuswali wanapofikisha miaka saba, wapigeni wanapofikisha miaka kumi na watenganishe baina yao katika malazi.”

Vilevile maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth Swahiyh:

”… mtoto mpaka abaleghe.”

haina maana kwamba ana jukumu juu ya matendo yake. Mtoto hawi mwenye kupata dhambi mpaka pale atapobaleghe. Hata hivyo mtoto katika kipindi hichi anatakiwa kuamrishwa swalah ili aweze kuzowea. Mpaka pale mtoto anapobaleghe anakuwa tayar amekwishaizowea.

[1] Abu Daawuud (495) na Ahmad (6756). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (1/266).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 63-64
  • Imechapishwa: 24/06/2018