03. Sababu Za Kupotea Kwa Ibn Laadin Na Wafuasi Wake


Kiongozi wa al-Qaa´idah Ibn Laadin na kundi lake kama ad-Dhwawaahiriy na Abu Musw´ab az-Zarqaawiy aliyeuawa kwenye fitina ya Iraaq na rafiki yake Muhammad al-Mas´ariy na Sa´d al-Faqiyh ambaye alikuwa anaishi kwenye nchi za kikafiri na za madhambi na kuita kujitolea muhanga kuwa ni shahada na kuwaahidi wale wenye kufanya hayo yale anayopata shahidi katika njia ya Allaah. Ni ubaya ulioje wa waliyoyasema na kuhukumu! Kwa sababu yanaenda kinyume na Shari´ah iliotakasika ambayo wanachuoni watukufu wanazungumza kwayo. Wanachuoni hawa wanamcha Allaah na hawamnasibishii Allaah wala Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa tu yaliyothibiti katika Qur-aan na Sunnah kwa ufahamu sahihi na sio kwa tafsiri mbovu, kama afanyavyo Ibn Laadin, Muhamamd al-Masw´ab, Sa´d al-Faqiyh na watu wa dhambi mfano wao. Watu hawa wanasema na kufanya mambo mengi yenye kwenda kinyume. Watu hawa wamefanya vitendo vya jinai vikubwa. Yote haya ima ni kutokana na ujinga wao mchafu na ukaidi wa wazi au ni chuki zao za wazi na angamivu walizo nazo wao wenyewe na wale wenye kuwatii na kuwanusuru kwa njia zote za kishetani. Wataulizwa kwayo siku ya Qiyaamah wakati watapoletwa mbele ya Allaah na Atamlipa kila mmoja kwa lile alilolifanya na kwa uadilifu.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Waqafaat wa Ma´aalim, uk. 10-11
  • Imechapishwa: 30/11/2014