Mwingi wa huruma (الرحمن) na Mwenye kurehemu (الرحيم) ni majina mawili ya Allaah (´Azza wa Jall) yaliyo na huruma. Huruma ni sifa ya Allaah. Kila moja katika majina hayo yamebeba sifa.

Mwingi wa huruma (الرحمن) ni rehema yenye kuenea juu ya viumbe wote.

Mwenye kurehemu (الرحيم) ni rehema maalum kwa waumini. Amesema (Ta´ala):

وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا

“Naye ni Mwenye kuwarehemu waumini.”[1]

Mwingi wa huruma (الرحمن) ni rehema yenye kuenea juu ya viumbe wote, wakiwemo makafiri na wanyama. Wanaishi kwa rehema za Allaah. Allaah amewepesisha mambo kati ya wao kwa wao kutokana na rehema Zake. Kwa hiyo ni rehema ilioenea kwa viumbe wote kwao kwa kwao. Mnyama anapandisha mguu wake asimkanyage mtoto wake kwa sababu ya kumuhurumia.

Mwenye kurehemu ni sifa miongoni mwa sifa za Allaah (´Azza wa Jall) inayolingana na utukufu Wake na sio kama rehema ya viumbe wengine. Ni kama sifa Zake zengine zote. Tunamsifu nayo kama Alivyojisifu Mwenyewe, lakini hatufananishi rehema Zake na rehema za viumbe Wake.

[1] 33:43

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 20
  • Imechapishwa: 06/08/2019