03. Ni lazima kwa waislamu kuonelea kuwa mayahudi na manaswara ni makafiri

Ni lazima kwa waislamu kuwakufurisha wale waliokufurishwa na Allaah na Mtume Wake, wabainishe batili zao na wawatahadharishe waislamu juu ya vitimbi vyao. Dini ya kiyahudi na dini ya kikristo zimekuwa ni dini batili na hivyo haijuzu kuzifuata na kubaki juu yake. Kwa sababu Allaah amezifuta kwa kule kumtumiliza Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), amewawajibishia watu na majini kumfuata na kushikamana na Shari´ah yake. Amesema (Ta´ala):

وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ يَأْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

”Rehema Yangu imekienea kila kitu. Basi nitawahukumia wale wenye kumcha Allaah na wanaotoa zakaah na ambao wao wanaziamini Aayah Zetu. Wale wanomfuata Mtume, Nabii asiyejua kuandika na kusoma, wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawraat na Injiyl anawaamrisha mema na anawakataza maovu na anawahalalishia vizuri na anawaharamishia vibaya na anawaondoshea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao. Basi wale waliomwamini na wakamtukuza na wakamnusuru na wakafata Nuru ambayo imeteremshwa pamoja naye – hao ndio wenye kufaulu.”[1]

Kwa hivyo kwa sababu ya Aayah hii wametoka nje ya Uislamu na ni miongoni mwa sababu za kufaulu mayahudi, manaswara na washirikina wengine wote. Hawakusifika kwa sifa hizi ambazo Allaah amewasifu kwazo wale waliofaulu. Bali wote wamemfanyia uadui, hawakumnusuru na wala hawakufuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye. Isipokuwa wachache walioongozwa na Allaah katika wao. Basi watu hao watakuwa pamoja na waislamu waliofaulu.

[1] 07:156-157

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/articles/78/الاسلام-هو-دين-الله-ليس-له-دين-سواه
  • Imechapishwa: 05/10/2021