03. Kuamini kuwa Allaah ndiye kaumba viumbe na ndiye anayewaendesha

Katika kumuamini Allaah (Subhaanah) kunaingia vilevile kuamini kuwa Allaah ndiye kaumba ulimwengu na ndiye Mwenye kuyaendesha mambo yao kwa ujuzi na uwezo Wake kama alivyotaka (Subhaanah). Vilevile kuamini kuwa Yeye ndiye mfalme wa dunia na Aakhirah na Mola wa walimwengu wote. Hakuna muumba mwingine asiyekuwa Yeye na hakuna Mola asiyekuwa Yeye. Amewatuma Mitume na akateremsha vitabu ili kuwatengeneza waja na kuwaita katika yatayowafanya kuokoka duniani na Aakhirah. Inatakiwa vilevile kuamini kuwa Yeye (Subhaanah) hana mshirika katika yote hayo. Amesema (Ta´ala):

اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ ۖوَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ

“Allaah ni Muumbaji wa kila kitu Naye juu ya kila kitu ni mdhamini anayetegemewa.” (39:62)

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi. Anafunika usiku kwa mchana, unaufuatia upesiupesi na jua na mwezi na nyota vyote vimetiishwa kwa amri Yake. Tanabahi! Ni Vyake pekee uumbaji na amri. Amebarikika Allaah, Mola wa walimwengu.” (07:54)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah as-Swahiyhah wa maa yudhwaadduhaa, uk. 06
  • Imechapishwa: 30/05/2023