03. Nafasi alionayo mwanamke katika kuiathiri jamii

Nadhani tutakuwa si wenye kukosea endapo tutasema kuwa utengenezaji wa nusu ya jamii au zaidi yake ni jukumu limemvaa mwanamke. Hilo ni kutokana na sababu mbili:

Ya kwanza: Wanawake wako idadi sawa na wanaume endapo watakuwa wao si wengi zaidi. Bali wao ndio wengi zaidi. Namaanisha kuwa kizazi cha Aadam wengi wao ni wanawake. Hivyo ndivyo imefahamisha Sunnah ya kiutume. Lakini hata hivyo inatofautiana kutoka nchi hadi nyingine, kutoka wakati hadi mwingine. Wanawake katika nchi fulani wanaweza kuwa wengi kuliko wanaume. Katika nchi nyingine mambo yanaweza pia kuwa kinyume na hivyo. Kadhalika wanawake katika wakati fulani wanaweza kuwa wengi kuliko wanaume. Katika wakati mwingine mambo yanaweza pia kuwa kinyume na hivyo. Kwa hali yoyote mwanamke ana jukumu kubwa katika kuitengeneza jamii. Kuna masuala mengine yanayobainisha umuhimu wa jukumu la mwanamke katika kuitengeneza jamii.

Ya pili: Kukuwa kwa vizazi mwanzoni wake kunakuwa mikononi mwa wanawake. Hapo ndipo kutabainika umuhimu wa yale ambayo ni wajibu kwa mwanamke katika kuitengeneza jamii.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dawr-ul-Mar´ah fiy Iswlaah-il-Mujtama´ https://www.sahab.net/home/?p=806
  • Imechapishwa: 02/02/2017