Alizaliwa ´Uyaynah mwaka wa 1115 na akakulia kwenye nyumba ya elimu, uongozi na utukufu. Baba yake ´Abdul-Wahhaab alikuwa ni mwanachuoni na hakimu. Babu yake Sulaymaan alikuwa ni Muftiy huko Najd na kiongozi wa wanachuoni wake. Ami zake na mabinamu zake walikuwa ni wenye vyeo vya juu na wenye elimu na vyeo. Mji wake wa ´Uyaynah na miji mingine pambizoni mwake ilikuwa imejaa wanachuoni ambao walikuwa na mafungamano yenye nguvu kabisa na wanachuoni wa Hanaabilah huko Shaam, Palestina na sehemu nyinginezo. Walikuwepo wanachuoni ambao ni mabingwa wa Fiqh.

Shaykh Muhammad alihifadhi Qur-aan akiwa bado mdogo. Alisoma Fiqh, tafsiri ya Qur-aan na Hadiyth kwa baba yake na waanchuoni wa mji wake. Baada ya mazingatio, majadiliano na mahakikisho haikuchukua muda mrefu mpaka akajifunza kutoka kwao. Baba yake, wanachuoni wake na marafiki zake wakapendezwa na kile walichokiona.

Kisha akataka kujizidishia elimu ambapo akaiendea Qur-aan, pamoja na tafsiri zake, kisomo chake, mazingatio na kuchuma hukumu, Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pamoja na historia yake. Alichuma faida za kiajabu kutoka kwenye Qur-aan na Sunnah ambazo baadaye aliziandika kwenye vitabu vyake, vijitabu vyake na fatwa zake. Alitilia bidii zaidi vitabu vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na Shaykh na Imaam Ibn-ul-Qayyim, khaswakhaswa vitabu vya ´Aqiydah.

Baadaye hima na malengo yake yaliongezeka ambapo akasafiri kwenda kwa wanachuoni wa Makkah na Madiynah, Ahsaa´ na Baswrah huko ´Iraaq. Akakutana nao na akajifunza elimu nyingi katika Fiqh na Hadiyth na elimu zake. Akakusanya elimu nyingi na akajifunza kwa kila ambaye aliweza kukutana naye. Sambamba na hilo akasoma vitabu vilivyoandikwa na maimamu wakaguzi, tafsiri ya Qur-aan na Hadiyth.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 11
  • Imechapishwa: 24/06/2019