03. Mfano wa jinsi wakristo wanavyopotosha Kitabu chao

Katika matayo 07:21 neno “Bwana” limefasiriwa kuwa ni “Mola/Mungu” ili kutaka kuwafanya watu waamini kuwa Masihi ndiye Allaah:

“21Si kila anambiaye ´Mungu, mungu` ataingia katika ufalme wa mbinguni, isipokuwa tu wale wafanyao matakwa ya Baba yangu aliye mbinguni.[1]

Lakini mwenye kuzingatia Aya iliyobaki ataona kuwa inathibitisha kuwa Masihi ni mwanadamu. Tafsiri sahihi ni:

“21Si kila anambiaye ´Bwana, bwana` ataingia katika ufalme wa mbinguni, isipokuwa tu wale wafanyao matakwa ya Baba yangu aliye mbinguni.”

Imeshatangulia ya kwamba Allaah sehemu nyingi kwenye Injili ameitwa “Baba” na sio jambo maalum kwa Masihi.

[1] Matayo 07:21

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Taqiyy-ud-Diyn al-Hilaaliy al-Maghribiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Baraahiyn al-Injiylyyah ´alaa anna ´Iysaa daakhil fiyl-´Ubuudiyyah wa la hadhdhwa lahu fiyl-Uluuhiyyah, uk. 13
  • Imechapishwa: 16/10/2016