Ilipokuwa kundi hili ndilo lililosalimika kutokamana na upotevu, jambo linapelekea kujua majina na alama zake ili mtu aweze kulifuata. Lina majina matukufu yanayolipambanua na mapote mengine. Miongoni mwa majina na alama muhimu zaidi ni: kundi lililookoka, pote lililonusuriwa na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Maana yake ni kama zifuatazo:

1 – Kundi lililookoka ina maana kwamba ni kundi lililookoka kutokamana na Moto pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipolibagua wakati alipokuwa anataja kuhusu mapote na akasema:

“Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.”

Bi maana [hili limoja] ndilo halitokuwa Motoni.

2 – Ni lenye kushikamana barabara na Qur-aan na Sunnah za Mtume wake na yale waliyokuwemo wale wa mwanzo waliotangulia ambao ni Muhaajiruun na Answaar pindi aliposema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu yao:

“Ni wale wataofuata yale ninayofuata mimi hii leo na Maswahabah zangu.”

3 – Watu wenye kundi hilo ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Wamejipambanua kwa sifa mbili kuu:

Sifa ya kwanza: Wameshikamana na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka watu wake wakawa hivo tofauti na mapote mengine ambapo wameshikamana na maoni, matamanio na maneno ya viongozi wao. Hayajinasibishi na Sunnah. Yamejinasibisha na Bid´ah na upotevu wake – mfano wa hao ni Qadariyyah na Murji-ah – au kwa viongozi wao – mfano wa hao ni Jahmiyyah – au kwa matendo yao machafu – mfano wa hao ni Raafidhwah na Khawaarij.

Sifa ya pili: Watu wa al-Jamaa´ah. Hili ni kwa sababu ya kukusanyika kwao juu ya haki na kutofarikiana kwao. Hili ni tofauti na mapote mengine. Wao hawakusanyiki juu ya haki. Bali wanakusanyika juu ya matamanio yao. Hakuna haki inayowakusanya.

4 – Ni kundi lililonusuriwa mpaka siku ya Qiyaamah kwa sababu limeinusuru dini ya Allaah na hivyo Allaah akalinusuru . Amesema (Ta´ala):

إِن تَنصُرُوا اللَّـهَ يَنصُرْكُمْ

“Mkimnusuru Allaah Naye atakunusuruni.”[1]

Kwa ajili hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu yake:

“Hawatodhurika na wale wenye kuwanyima nusura na wenye kwenda kinyume nao mpaka kifike Qiyaamah ilihali bado wako katika hali hiyo.”[2]

[1] 47:07

[2] al-Bukhaariy (7311), Muslim (5059), Abu Daawuud (4654), at-Tirmidhiy (6669), Ibn Maajah (06) na Ahmad (04/97).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Usuwl ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 13-15
  • Imechapishwa: 12/05/2022