Kwa nini wakaitwa kwa jina hili? Jina la “Suufiyyah” limetoka katika jina la kigiriki “Sofia” na maana yake ni hekima. Imesemekana vilevile kwamba ni nisba ya nguo za pamba. Jina hili ndio liko karibu na usahihi, kwa kuwa nguo ya pamba ilikuwa ndio alama ya kuipa nyongo dunia (az-Zuhd). Inasemekana kwamba hili lilifanywa kwa ajili ya kujifananisha na ´Iysaa bin Maryam (´alayhis-Salaam). Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amepokea katika “Majmuu´-ul-Fataawaa” ya kwamba Muhammad bin Siyriyn alifikiwa na khabari kwamba kuna watu ambao wanazipa kipaumbele nguo za pamba kwa ajili ya kujifananisha na ´Iysaa bin Maryam (´alayhis-Salaam). Hivyo akasema:

“Kuna watu ambao wamependekeza kuvaa nguo za pamba na wanadai kwamba wanataka kujifananisha na ´Iysaa bin Maryam. Lakini uongofu wa Mtume wetu ni wenye kupendeza zaidi kwetu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akivaa nguo za pamba na nyenginezo.”[1]

[1] (07/11).

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqiyqat-us-Suufiyyah
  • Imechapishwa: 10/12/2019