Swali 3: Tunataraji kutuwekea wazi maana ya msemo “Fiqh-ul-Waaqiy´ (uelewa wa mambo ya kisasa) kwa kuzingatia ya kwamba tamko hili linaposemwa kunakusudiwa maana ya kilugha na si maana ya Kishari´ah?

Jibu: Imezoeleka kusemwa ni vigumu kuweka wazi jambo lililo wazi. Uelewa unaotakikana na uliopendekezwa ni ule wenye kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Huu ndio uelewa unaotakikana.

Ama kuhusu uelewa wa kilugha, ni katika mambo yaliyoruhusiwa. Hata hivyo sio jambo linalotakikana kwa watu. Kuelewa maana ya kilugha ni kule kujua maana ya maneno, machimbuko yake, herufi zake na kadhalika. Huu ndio huitwa uelewa wa kilugha. Kwa mfano ath-Tha´aalabiy na vitabu vingine vimeitwa “Fiqh-ul-Lughah”. Haya ni mambo yanayoitimiza mada.

Wakati neno “Fiqh” linapotajwa kama ilivyo katika maneno ya Allaah (Ta´ala):

لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ

“… ili wajifunze dini… ”[1]

فَمَالِ هَـٰؤُلَاءِ الْقَوْمِ لَا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ حَدِيثًا

“Basi wana nini hawa watu hawakaribi kufahamu yenye kuendelea?”[2]

وَلِلَّـهِ خَزَائِنُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَـٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَفْقَهُونَ

“Na ni za Allaah pekee hazina za mbingu na ardhi, lakini wanafiki hawafahamu.”[3]

na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule ambaye Allaah anamtakia kheri, basi humpa ufahamu akaielewa dini.”[4]

makusudio ya uelewa ni uelewa katika dini kwa kuzijua zile hukumu za Kishari´ah. Hili ndio lenye kutakikana. Haya ndio ambayo waislamu wanatakiwa kuyatilia umuhimu na kujifunza nayo.

Licha ya hivyo ni kwamba watu hawa hawakusudii uelewa wa kilugha wakati wanapozungumzia Fiqh-ul-Waaqiy´. Makusudio yao ni mtu ajishughulishe na mambo ya siasa na hamasa za kisiasa na kuweka wakati wote katika siasa.

Kuhusiana na uelewa wa hukumu, wanaita kuwa ni “uelewa wa sehemu tu” na “uelewa wa hedhi na nifasi” ili kuchokoza na kuwakimbiza watu mbali nayo[5].

[1] 09:122

[2] 04:78

[3] 63:07

[4] al-Bukhaariy (71) na Muslim (1037).

[5] Hili limebainisha kwamba Fiqh (uelewa) inayotakikana imegawanyika sampuli mbalimbali:

1 – Fiqh kwa maana ya kwamba mtu akaifahamu Qur-aan na Sunnah na kutoa hukumu katika viwili hivyo.

2 – Fiqh katika lugha ya kiarabu kama sarufi, mofotojia, balagha, etimolojia na semantiki.

3 – Fiqh katika mambo yenye kutatiza na matukio ili kuweza kutumia juu yake hukumu ya Shari´ah sahihi.

Ama yale wanayoita “Fiqh-ul-Waaqiy´”, makusudio ni kutaka kuwahamasisha watu na siasa, kuwakosoa watawala, kuchochea fitina na ghasia na kuyumbisha usalama. Wameyaita mambo haya jina hili ili kutaka kuwatia watu mchanga wa machoni. Hili sio jambo jipya kwa watu wa “Fiqh-ul-Waaqiy´. Mrithi na kiongozi wao Sayyid Qutwub alitumia jina hilo katika kitabu chake “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” wakati wa maneno ya Allaah (Ta´ala):

قَالَ اجْعَلْنِي عَلَىٰ خَزَائِنِ الْأَرْضِ ۖ إِنِّي حَفِيظٌ عَلِيمٌ

“Akasema: “Niweke katika hazina ya nchi; hakika mimi ni mhifadhi mjuzi.” (12:55)

na kusema:

“Uelewa wa Kiislamu umejitokeza katika jamii ya Kiislamu na kupitia harakati hizi za kijamii wakati inapokabiliwa na hali ya Kiislamu ya kisasa kila siku… Fiqh-ul-Harakah (uelewa wa harakati) inatofautiana ya harakati za kwenye karatasi… Fiqh-ul-Harakah (uelewa wa harakati) inatunza hali ya kisasa ambayo maandiko [ya Qur-aan na Sunnah] yameteremshwa kwa ajili yake na hukumu zikaundwa kwa ajili yake.” (04/2006)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 18/02/2017