03. Maana ya neno Fiqh-ul-Waaqi´


Swali 3: Tunataraji kutuwekea wazi maana ya msemo “Fiqh-ul-Waaqi´ (uelewa wa mambo ya kisasa) kwa kuzingatia ya kwamba tamko hili linaposemwa kunakusudiwa maana ya kilugha na si maana ya Kishari´ah?

Jibu: Imezoeleka kusemwa ni vigumu kuweka wazi jambo lililo wazi. Uelewa unaotakikana na uliopendekezwa ni ule wenye kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Huu ndio uelewa wenye kutakikana.

Ama kuhusu uelewa wa kilugha, imeruhusiwa. Hata hivyo sio jambo linalotakikana kwa watu. Kuelewa maana ya kilugha ni kule kujua maana ya maneno, mizizi yake, herufi zake na kadhalika. Huu ndio unaitwa uelewa wa kilugha. Kwa mfano ath-Tha´aalabiy na vitabu vingine vimeitwa “Fiqh-ul-Lughah”. Haya ni mambo yanayoitimiza mada.

Wakati neno “Fiqh” linapotajwa kama ilivyo katika Kauli ya Allaah (Ta´ala):

لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ

“… wajifunze dini… ” (09:122)

فَمَالِ هَـٰؤُلَاءِ الْقَوْمِ لَا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ حَدِيثًا

“Basi wana nini hawa watu hawakaribi kufahamu yenye kuendelea?” (04:78)

وَلِلَّـهِ خَزَائِنُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَـٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَفْقَهُونَ

“Na ni za Allaah Pekee hazina za mbingu na ardhi, lakini wanafiki hawafahamu.” (63:07)

na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule ambaye Allaah Anamtakia kheri, basi humfanya akaielewa dini.”[1]

makusudio ya uelewa ni uelewa katika dini kwa kujua hukumu za Kishari´ah. Hili ndio lenye kutakikana. Haya ndio ambayo waislamu wanatakiwa kuyatilia umuhimu na kujifunza.

Licha ya hivyo ni kwamba watu hawa hawakusudii uelewa wa kilugha wakati wanapozungumzia Fiqh-ul-Waaqi´. Makusudio yao ni mtu ajishughulishe na mambo ya siasa na hamasa za siasa na kuweka wakati wote wenye siasa.

Kuhusiana na uelewa wa hukumu, wanaita kuwa ni “uelewa wa sehemu kidogo” na “uelewa wa hedhi na nifasi” ili kuchokoza na kuwakimbiza watu nayo[2].

[1] (al-Bukhaariy (71) na Muslim (1037).)

[2] Hili limeweka wazi juu ya kwamba kuna Fiqh (uelewa) sampuli tatu unaotakikana:

1- Fiqh kwa maana ya kwamba mtu akaifahamu Qur-aan na Sunnah na kutoa hukumu kwenye hayo.

2- Fiqh katika lugha ya kiarabu kama nahuw, sarufi na balagha na kisasili na semantiki yavyo.

3- Fiqh katika mambo yenye kutatiza na ajali ili kuweza kutumia hukumu ya Kishari´ah na ilio sahihi.

Kuhusiana na yale wanayoita “Fiqh-ul-Waaqi´”, makusudio ni kutaka kuwahamasisha watu na siasa, kuwakosoa watawala, kuchochea fitina na ghasia kutingisa usalama. Wameita mambo haya jina hili ili kutaka kuwatia watu mchanga machoni. Hili sio jambo jipya kwa watu wa “Fiqh-ul-Waaqi´. Mrithi na kiongozi wao Sayyid Qutwub alitumia jina hilo katika kitabu chake “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” katika Kauli ya Allaah (Ta´ala):

قَالَ اجْعَلْنِي عَلَىٰ خَزَائِنِ الْأَرْضِ ۖ إِنِّي حَفِيظٌ عَلِيمٌ

“Akasema: “Niweke katika hazina ya nchi; hakika mimi ni mhifadhi mjuzi.” (12:55)

na kusema:

“Uelewa wa Kiislamu umejitokeza katika jamii ya Kiislamu na kupitia harakazi hizi za kijamii wakati inapokabiliwa na hali ya Kiislamu ya kisasa kila siku… Fiqh-ul-Harakah (uelewa wa harakati) inatofautiana ya harakati za kwenye karatasi… Fiqh-ul-Harakah (uelewa wa harakati) inatunza hali ya kisasa ambayo maandiko [ya Qur-aan na Sunnah] yameteremshwa kwa ajili yake na hukumu zikaandaliwa kwayo.” (04/2006)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Adjwibah al-Mufiydah ´an As'ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 18/02/2017