03. Kumuomba asiyekuwa Allaah ni shirki kubwa

Miongoni mwa hayo ni shirki kubwa na ndogo. Shirki kubwa ni kama mfano wa kumuomba asiyekuwa Allaah katika mawalii, watu wema, wafu na wengineo. Kwa kuwa du´aa ndio ´ibaadah. Bi maana ndio aina kubwa ya ´ibaadah. Ndani yake kumekusanywa ´baadah nyingi ikiwa ni pamoja na unyenyekevu, kujidhalilisha kwa Allaah, kutambua ya kuwa hakuna anayenufaisha wala kudhuru ila Allaah pekee, kumtegemea Allaah na kurejea kwa Allaah. Du´aa inakuwa na mambo yote haya. Kwa ajili hii, ndio maana amesema (Jalla wa ´Alaa):

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا

“Kwamba sehemu zote za kuswalia ni kwa ajili ya Allaah, hivyo basi msiombe yeyote pamoja na Allaah.” (72:18)

Amesema (Subhaanah):

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ

“Mola wenu anasema: “Niombeni Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari na ‘ibaadah Yangu, watauingika [Moto wa] Jahanam wadhalilike.” (40:60)

Amesema (Ta´ala):

فَادْعُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ

“Basi mwombeni Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini, japokuwa wanachukiwa makafiri.” (40:14)

Du´aa umuhimu wake ni mkubwa. Wako watu wengi wanaomba badala ya Allaah katika mambo muhimu, ya kutia huzuni na shida mbalimbali. Wanaomba, wanaita na wakitafuta uokozi kwa asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ni azima kwa muislamu kutanabahi jambo hili. Hakika ni jambo la khatari sana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah al-Islaamiyyah as-Swahiyhah https://www.youtube.com/watch?v=KqoTCYds6Cs&t=13s
  • Imechapishwa: 28/01/2019