03. Kitabu chako ni kama viungo vya mwili wako    

Kitabu cha mwanafunzi kinakumbushia zaidi kiungo cha mwili wake. Mwanafunzi anaishi kwa msaada wa kitabu chake. Vitabu ndio usikizi na uoni wake; akivikosa elimu yake inadhoofika hatua kwa hatua. Utaona namna ambavyo yule ambaye anafanya mchezo na kusoma na elimu anadhoofika na kusahau elimu kidogo kidogo mpaka anakuwa mtu ambaye si msomi kadri muda unavyokwenda.

Kusoma vitabu ni jambo la muhimu sana. Hili linahitajia mwanafunzi awe na mafungamano yenye nguvu kabisa na kitabu. Mafungamano haya yana adabu zake, uzuri wake na masharti yake, ambayo yamebainishwa na wanachuoni katika vitabu vyao ikiwa ni pamoja vilevile na kitabu “Jaami´ Bayaan-il-´Ilm wa Fadhwlih” cha Ibn ´Abdil-Barr na “Tadhkirat-us-Saami´ wal-Mutakallim” cha Ibn Jamaa´ah.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Twaalib-ul-´Ilm wal-Kutub
  • Imechapishwa: 03/05/2020