03. Katika Sunnah ni kushikamana na al-Jamaa´ah

Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

2- Ni katika Sunnah kulazimiana na al-Jamaa´ah. Ambaye hataki kuwa katika al-Jamaa´ah na akafarikiana nayo, basi ameivua kamba ya Uislamu katika shingo yake na atakuwa ni mpotevu mwenye kupoteza.

Maadamu mambo ni kama mlivyosikia ya kwamba Uislamu ndio Sunnah na Sunnah ndio Uislamu. Sunnah ni aina mbalimbali. Sasa ameanza kufafanua. Kwanza ameanza kusema kwa jumla kisha baadae akaanza kupambanua.

Katika Sunnah ni kushikamana na al-Jamaa´ah ya Waislamu. Makusudio ya “al-Jamaa´ah” ni mkusanyiko wa Waislamu ambao uko juu ya haki. Ama makundi yasiyokuwa juu ya haki, haya hayaitwi kuwa ni al-Jamaa´ah. Kila kundi ambalo limekusanyika juu ya upotevu au juu ya mfumo unaokwenda kinyume na Uislamu au juu ya njia inayokwenda kinyume na Uislamu, haliitwi kuwa ni al-Jamaa´ah. Makusudio ya al-Jamaa´ah hapa ni Ahl-ul-Haqq. Sio lazima wawe wengi, bali lau akiwa ni mtu mmoja tu aliye juu ya haki, basi anaitwa kuwa ni al-Jamaa´ah. al-Jamaa´ah ni kushikamana na haki, ni mamoja watu wake wawe wachache au wengi. Hii ndio al-Jamaa´ah. Usende kinyume na al-Jamaa´ah iliyo juu ya haki. Bali unapaswa kuwa pamoja nao katika Kunakuja bayana huko mbele kuhusu anayekwenda kinyume na al-Jamaa´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 15
  • Imechapishwa: 13/06/2017