Allaah amemdhamini yule mwenye kuwafuata al-Muhaajiruun na al-Answaar kwa wema… ni lazima ipatikane sharti hii na isiwe ni madai tu. Sio mtu kujiita au kujinasibisha tu pasi na ujuzi, ima mtu akafanya hivo kwa ujinga au kwa matamanio. Sio kila mwenye kujinasibisha na Salaf anakuwa Salafiy, mpaka awe anawafuata kwa wema. Hii ni sharti iliyowekwa na Allaah (´Azza wa Jall).

Hii inatakikana kwa wafuasi wausome mfumo wa Salaf, wautambue na washikamane nao barabara. Kujinasibisha nao tu na wakati huo huo mtu akawa hajui mfumo wala madhehebu yao, hili halifidishi kitu. Huyu si katika Salaf na wala sio Salafiy. Hakuwafuata Salaf kwa wema kama Allaah (´Azza wa Jall) alivyoshurutisha. Nyinyi katika chuo kikuu hichi, katika nchi hii na katika misikiti ya nchii hii kinachofunzwa ni mfumo wa Salaf-us-Swaalih. Lengo ni ili mtu aweze kuwafuata kwa wema. Haihusiani na madai na kujiita. Ni wangapi wamedai kuwa ni Salafiyyah na kwamba wanafuata mfumo wa Salaf ilihali uhalisia wa mambo ni kwamba sivyo. Hili ni kutokana ima na kutokujua kwake mfumo wa Salaf au kwa sababu ya kufuata matamanio yake; mtu akawa anajua lakini hata hivyo akawa anafuata matamanio yake badala ya kufuata mfumo wa Salaf.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com