03. Hivi ndivo yanavothibitishwa maneno ya Allaah

25 – Maneno kwa herufi yanapaswa kuthibitishwa, sauti, lugha, maneno na surah.

26 – Maneno Yake kumzungumzisha Jibriyl na Malaika.

27 – Maneno Yake kumzungumzisha Malaika wa kifuko cha uzazi na Malaika wa kutoa roho.

28 – Maneno Yake kumzungumzisha Ridhwaan na Maalik.

29 – Maneno Yake kumzungumzisha Aadam, Muusa, Muhammad na waliokufa mashahidi.

30 – Maneno Yake kuwazungumzisha waumini wakati wa Hesabu na Peponi.

31 – Kushuka kwa Qur-aan katika mbingu ya chini.

32 – Qur-aan ndio iliyoandikwa ndani ya Misahafu.

33 – Anapenda baadhi ya visomo, Anachukia vyengine.

34 – Imekuja katika Hadiyth:

”Allaah hasikizi kitu kama anavomsikiza Nabii Wake anayesoma Qur-aan kwa sauti nzuri kabisa.”[1]

35 – Imekuja katika Hadiyth:

”Allaah anamsikiza zaidi msomaji Qur-aan kuliko bwana wa mjakazi anavosikiliza nyimbo ya mjakazi wake.”[2]

[1] al-Bukhaariy (5023-5024) na Muslim (792).

[2] Ibn Maajah (1340) na al-Haakim (2097). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Ibn Maajah” (251).

  • Mhusika: Imaam Abul-Qaasim Sa´d bin ´Aliy bin Muhammad az-Zinjaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ajwibah fiy Usuul-id-Diyn, uk. 73-81
  • Imechapishwa: 14/06/2021