Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) aliulizwa kuhusu mwanaume ambaye yuko na mke. Mke huyo anafunga mchana na anasimama usiku kuswali. Kila wakati mume wake anamwita kitandani anamkatalia na anatanguliza jambo la kuswali usiku na kufunga mchana juu ya kumtii mume wake. Je, inafaa kwake kufanya hivo? Akajibu kwa kusema:

“Si halali kwake kufanya hivo kwa maafikiano ya waislamu. Bali ni lazima kwake kumtii wakati atapomwita kitandani, jambo ambalo ni faradhi na wajibu kwake. Kuhusu kusimama usiku kuswali na kufunga mchana ni mambo yaliyopendekezwa. Ni vipi muumini wa kike atatanguliza ´ibaadah inayopendeza kabla ya ´ibaadah ya faradhi?”[1]

Akaendelea kusema:

“Baada ya haki ya Allaah na Mtume Wake mwanamke hana haki ambayo imefanywa lazima zaidi kushinda haki ya mume.”

Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu  ´alayhi wa sallam) amesema:

“Endapo mwanamke angejua haki ya mume, basi asingekaa chini wakati anakula chakula chake cha jioni au cha mchana mpaka atakapomaliza.”[2]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (32/274-275).

[2] al-Bazzaar (01/180 – Kashf) na wengineo. Ipo katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´ as-Swaghiyr” (5135).

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 11-12
  • Imechapishwa: 19/09/2022