03. Hadiyth “Watu wanne thawabu zao zinaendelea baada ya kufa… “

114- Imepokelewa kutoka kwa Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu wanne thawabu zao zinaendelea baada ya kufa: mtu anayekufa hali ya kuwa analinda mipaka ya taifa katika njia ya Allaah, mtu ambaye amefunza elimu (ujira wake unaendelea muda wa kuwa elimu ile inatendewa kazi), mtu ambaye ametoa swadaqah (analipwa ujira muda wa kuwa swadaqah hiyo ni yenye kuendelea) na mtu aliyeacha mtoto mwema anayemuombea du´aa.”[1]

Ameipokea Ahmad, al-Bazzaar ba at-Twabaraaniy katika ”al-Kabiyr” na ”al-Awsatw”. Ni Swahiyh.

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/157)
  • Imechapishwa: 03/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy