107- Jaabir ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Usijifunze elimu kwa ajili ya kujifakharisha kwa wanachuoni, kugombana na wapumbavu wala kwa ajili ya kuingia katika vikao vizuri. Yule mwenye kufanya hivo basi ajihadhari na Moto ajihadhari na Moto.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah, Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” na al-Bayhaqiy kupitia kwa Yahyaa bin Ayyuub al-Ghaafiqiy, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Abuz-Zubayr. Yahyaa huyu ni mwaminifu na al-Bukhaariy na Muslim wote wawili wamemjengea hoja na wala hayazingatiwi maoni ya wale wenye kumdhoofisha.

108- Ibn Maajah amepokea mfano wake kupitia kwa Hudhayfah.[2]

[1] Swahiyh kupitia zengine.

[2] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/153)
  • Imechapishwa: 03/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy