718- Ibn Khuzaymah amepokea katika ”as-Swahiyh” yake kupitia kwa Abu Dharr ambaye amesema:

”Niliingia msikitini siku ya ijumaa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yuko anakhutubu. Nikakaa karibu na Ubayy bin Ka´b. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasoma Suurah ”at-Tawbah” ambapo nikamwambia Ubayy: ”Ni lini iliteremka Suurah hii?” Akanitazama kwa ukali na hakunisemesha kitu. Nikakaa baada ya muda kidogo nikamuuliza tena ambapo akanitazama kwa ukali na hakunisemesha kitu.  Nikakaa baada ya muda kidogo nikamuuliza tena ambapo akanitazama kwa ukali na hakunisemesha kitu. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomaliza kuswali nikamwambia Ubayy: ”Nilikuuliza ambapo ukanitazama kwa ukali na hukunisemesha kitu.” Ubayy akasema: ”Huna katika swalah yako isipokuwa kile ulichofanya upuuzi.” Nikaenda kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumwambia: ”Ee Mtume wa Allaah! Niliketi karibu na Ubayy wakati ulipokuwa ukisoma at-Tawbah. Nikamuuliza: ”Ni lini iliteremka Suurah hii?” Akanitazama kwa ukali na hakunisemesha kitu. Kisha akanambia: ”Huna katika swalah yako isipokuwa kile ulichofanya upuuzi.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ubayy amesema kweli.”[1]

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/447)
  • Imechapishwa: 14/01/2018