147- Ibn ´Abbaas ameeleza kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Tahadharini na sehemu tatu zilizolaaniwa. Kukasemwa: “Ni zipi sehemu tatu hizo zilizolaaniwa, ee Mtume wa Allaah? Akasema: “Mmoja wenu akikidhi haja katika kivuli kinachotumiwa, katika njia au karibu na maji.”[1]

Ameipokea Ahmad.

[1] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/171-172)
  • Imechapishwa: 10/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy